Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasili katika hospitali ya Rufaa ya Mikoa ya Kanda ya Kusini inayojengwa katika eneo la Mitengo Mtwara Mikindani ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa hapitali hiyo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipokea maelezo kutoka kwa Meneja Mradi wa Ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mikoa ya Kanda ya Kusini inayojengwa katika eneo la Mitengo Mtwara Mikindani.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akifafanua jambo alipotembelea hospitali ya Rufaa ya Mikoa ya Kanda ya Kusini inayojengwa katika eneo la Mitengo Mtwara Mikindani.
Mwonekano wa eneo la ujenzi la hospitali ya Rufaa ya Mikoa ya Kanda ya Kusini inayojengwa katika eneo la Mitengo Mtwara Mikindani.
Na Mwandishi wetu Mtwara.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ametembelea hospitali ya Rufaa ya Mikoa ya Kanda ya Kusini inayojengwa katika eneo la Mitengo Mtwara Mikindani ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa hapitali hiyo.
Akiwa katika eneo la ujenzi Waziri Mwalimu amewataka viongozi wa Mkoa pamoja na wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa hospitali hiyo kubwa kwa Mikoa ya Kusini na kuwashauri kufikiria namna ya bora ya kuboresha manzari ya hospitali hiyo ili pia iweze kuvutia wagonjwa wa nje kutumia hospital hiyo.
‘’Tunataka kuondokana na mtindo wa zamani wa ujenzi wa hospitali na kujenga hospitali za kisasa zenye huduma za hotel kama ilivyo hospital ya Apolo Nchini India ambapo wagonjwa wanaoenda kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo ukaa hotelini .” Aliongeza Waziri Mwalimu.
Waziri Mwalimu alivutiwa na manzari ya eneo hospital hiyo inapojengwa kwa kuwa na upande mmoja unaoelekea katika bahari jambo ambalo linafanya aeneo hilo kuwa na mvuto wa kipekee.
Hospitali hiyo imepangwa kukamilika ifikapo mwezi wa nane mwaka 2020 na itakuwa hospitali kubwa ya Rufaa itakayotumiwa na Mikoa ya Kusini ambayo ni Mikoa ya Songea, Lindi na Mtwara ikiwemo pia sehemu za mkoa wa Pwani na mikoa jilani.
Waziri Mwalimu yuko Mkoani Mtwara kuungana na Wazee wote Nchini kusherekea Maadhimisho ya Kimataifa ya Siku ya Wazee Duniani yanayoadhimishwa Kitaifa Mkoani Mtwara kwa Siku tatu kuanzia Septemba 29, na kufikia kilele chake Octoba 1, 2019.