Muonekano wa Kivuko kipya cha Kayenze Bezi ambacho ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu, kivuko hicho kimegharimu jumla ya shilingi Bilioni 2.7 za Kitanzania na kitatoa huduma kati ya Kayenze na Bezi Wilaya ya Ilemela mkoa wa Mwanza
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akitoa taarifa fupi wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TEMESA Profesa Idriss Mshoro kulia ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko viwili vipya vya Chato Mharamba na Bugorola Ukara vinavyogharimu jumla ya shilingi bilioni 7.3 za Kitanzania. Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella.
Meneja wa Kampuni ya Songoro Major Songoro (wa pili kushoto) akimpa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella katikati wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko viwili vipya vya Chato Mharamba na Bugorola Ukara vinavyogharimu jumla ya shilingi bilioni 7.3. Wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle na Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TEMESA Profesa Idrissa Mshoro.
Meneja wa Kampuni ya Songoro Major Songoro kulia akimpa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongella wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko viwili vipya vya Chato Mharamba na Bugorola Ukara vinavyogharimu jumla ya shilingi bilioni 7.3 za Kitanzania.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA)
……………………
NA ALFRED MGWENO- TEMESA MWANZA
Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) inatarajiwa kukamilisha ujenzi wa vivuko viwili vipya vinavyogharimu jumla ya shilingi bilioni 7.3 ifikapo mwezi Februari mwaka 2020.
Hayo yamebainishwa leo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala huo Profesa Idrissa B. Mshoro alipotembelea yadi ya Songoro Ilemela jijini Mwanza kukagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko hivyo unaoendelea katika karakana hiyo ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella alialikwa kushuhudia ukaguzi huo.
Mhandisi Maselle alisema mkataba kwa ajili ya ujenzi wa kivuko cha Bugorola Ukara ulisainiwa Tarehe 8 mwezi Februari mwaka huu wakati ule wa Chato Mharamba ulisainiwa Tarehe 15 mwezi Aprili na ujenzi wa vivuko vyote unafanywa na kampuni hiyo ya kizalendo ya Songoro Marine.
‘’Ujenzi wa kivuko cha Bugorola una gharama ya shilingi za Kitanzania bilioni 4.2 wakati ule wa Chato Nkome ni wa shilingi bilioni 3.1 bila VAT na fedha zote hizi zinatolewa na serikali ya Tanzania.’’ Alisema Mtendaji Mkuu.
Aliongeza kuwa Wakala unaendelea na ukarabati mkubwa wa kivuko cha MV. Sengerema kwa gharama ya shilingi milioni 689.4 na utakamilika ifikapo mwezi Novemba mwaka huu huku ule wa kivuko cha Kayenze Bezi unaogharimu bilioni 2.7 ukitara jiwa kukamilika ifikapo mwezi Novemba.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala huo Profesa Idrissa B. Mshoro akizungumza katika ziara hiyo alisema ununuzi wa vivuko hivyo ni jitihada za serikali katika kuboresha huduma kwa wananchi na kuhakikisha maeneo mengi ya nchi yanafikika kirahisi ili kuinua uchumi wa nchi hasa katika kulenga kufikia malengo ya nchi ya uchumi wa kati kufikia 2025.
‘’Naomba niishukuru serikali tena kwa kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa vivuko hivi ambavyo vitakuwa ni mkombozi kwa wananchi wa maeneo hayo kwani vitawaondolea adha ya usafiri waliyonayo kwa sasa hasa wananchi wenye kipato cha chini na mimi na bodi yangu tutahakikisha tunaisimamia vizuri TEMESA ili kutimiza malengo hayo.’’ Alisema Profesa Mshoro.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza katika ziara hiyo aliishukuru serikali kwa kuendelea kurahisisha usafiri wa vivuko katika mkoa huo ambapo vivuko vyote vikikamilika vitafanya idadi ya vivuko katika mkoa huo kutoka 11 na kufikia 14 ikiwemo boti moja ya uokozi ya (SAR II).
‘’Nichukue fursa hii kuwapongeza TEMESA kwa usimamizi mzuri na kazi nzuri wanayoifanya katika kuboresha miundombinu ya vivuko kote nchini.’’ Alisema Mhe. Mongella.
Kukamilika kwa miradi hii mipya ya vivuko kutaifanya TEMESA kutoka kuwa na vivuko 30 na kufikia kuwa na jumla ya vivuko 34 nchi nzima.