Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
MFUKO wa balozi wa Marekani wa kupambana na VVVU/Ukimwi umekabidhi ruzuku ya zaidi ya USD 257 sawa na zaidi ya sh. Milioni 574 kwa asasi 11 za kiraia zilizosajiliwa, ambazo hazijiendeshi kibiashara wala kidini kutoka maeneo mbali mbali nchini Tanzania ili kutekeleza miradi mbali mbali ya Ukimwi nchini.
Akizungumza katika hafla ya utoaji ruzuku hizo iliyoyafanyika American Corner katika Maktaba ya Taifa jijini Dar es Salaam leo Oktoba Mosi 2019, Kaimu Balozi wa ubalozi wa Mrekani, Dk, Inmi Patterson amesema, asasi zilizopokea ruzuku leo ni moja kati ya mashirika bora katika waliobora ambao maandiko yao yalikuwa na ushaiwishi mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii kusaidia watu wanaoishi na VVU na walio katika hatari zaidi kwenye maeneo hatarishi ya kupata Ukimwi.
Amesema, fedha hizo zinazotoka katika mfuko wa dharura wa rais wa marekani kwa ajili ya kupambana na Ukimwi (PEPFAR), zitasaidia pia asasi hizo kupigana vita dhidi ya unyanyapaa na ubaguzi uliopo kwenye VVU na Ukimwi na kuongeza ufahamu kuhusu tiba kupitia dawa za za mwanza za kupunguza kasi ua kuenea kwa virusi vya Ukimwi mwilini (TLD).
Amesema, katika mwaka huu wa 2019, walipokea maomb i223 kutoka katika mashirika mbali mbali ya asasi za kiraia na taasisi za dini lakini mashirika yaliyofanikiwa kupita ni 11 tu.
“Vikundi hivi 11 vinaujasiri na vinasimama kupigana vita dhidi ya unyanyapaa na ubaguzi uliopo kwenye VVU na Ukimwi”, amesema balozi Patterson.
Amesema watunukiwa wa ruzuku hiyo, walipendekeza miradi inayolenga kuongeza uelewa juu ya VVU, kuimarisha upatikana wa huduma kwa watu wanaoishi na VVU, yatima na watoto waishio katika mazingira hatarishi, makundi maalumu yaliyo katka hatari ya kupata na kuambukiza Ukimwi, wanaume na vijana balehe.
“Mashirika haya pia yanafahamu kuwa, watu wote wakiwamo wanaoishi na VVU anastahili kwenda katika vituo vya afya na zahanati zinazojitosheleza na ambazo zinatoa huduma bila ubaguzi kwani watu wanaoishi na VVU wanaweza kuishi Maisha ya kawaida kma watu wengine ili mradi wanaendelea kudumisha matumizi ya dawa.
Aidha Balozi Patterson ametoa wito kwa wanaume kujiyokeza kwa wingi na kwenda kupima ili wajue afya zao na siyo kuwaachia wanawake kwanza ndio wawe wakitangulia. Pia ameziaza asasi zote zilizopata ruzuku, kuendleza jitihada wanazozifaya ili kuweza kuleta mabadiliko.
Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Dar Inmi Patterson (kulia) akikabidhi cheti kwa kiongozi wa Parakuiyo Pastoralists Indigenous Community Development Organization (PAICODEO) Adam Ole Mwarabu jijini Dar es Salaam jana wakati wa hafla ya kukabidhiwa fedha kutoka mfuko wa Balozi wa Marekani kwa ajili ya kupambana na VVU/UKIMWI kwa ajaili ya Asasi za kiraia katika mapambano ya kudhibiti ukimwi kitaifa. Kushoto ni Afisa wa Fedha wa Asasi hiyo, Boriyai Kimjaa.
Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Dar Inmi Patterson (kulia) akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Tanzania Network of Women living with HIV and AIDS (TNW+) Joan Chamungu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhiwa fedha kutoka mfuko wa Balozi wa Marekani kwa ajili ya kupambana na VVU/UKIMWI kwa ajaili ya Asasi za kiraia katika mapambano ya kudhibiti ukimwi kitaifa. Kushoto ni Afisa wa Fedha wa Asasi hiyo, Michael Paul.
Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Dar Inmi Patterson (katikati) akiongoza kupiga picha ya pamoja na viongozi na wawakilishi wa Asasi za Kirai 11 zilizopatiwa fedha jumla ya Shilingi 574 Milioni wakati wa hafla ya kukabidhiwa fedha hizo kutoka mfuko wa Balozi wa Marekani kwa ajili ya kupambana na VVU/UKIMWI kwa ajaili ya Asasi za kiraia katika mapambano ya kudhibiti ukimwi kitaifa.