Wafanya kazi wa Kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania wamemuanga Mkurungenzi wao anayeondoka kwa njia ya kipekee baada ya kuhudumu kwenye kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka sita.
Akiongea kwenye hafla hiyo, Mkurungenzi huyo anayeondoka Bw. Sunil Colaso alisema kuwa Tanzania imekuwa ni kama nyumbani na hatua hii ya kuwaanga ni ngumu kwani kwa kipindi cha miaka sita Tanzania imekuwa ni nyumbani.
“Nachukua fursa hii kuwashukuru wafanya kazi wote wa Airtel kwa muda wote tuliofanya kazi pamoja. Tumeshirikiana kufanya kazi kwa bidii na umoja wenu ulifanya kazi yangu kuwa rahisi na kufanikisha malengo yetu. Ni Imani yangu kuwa kuwa leo wakati naondoka ninaacha nyuma timu imara ambayo itaendelea kuwahudumia Watanzania kwa huduma bora za mawasiliano kila siku.
Alitoa wito kwa wafanya kazi na wadau wengine kumuunga mkono Mkurugenzi mpya George Mathen anayetarajiwa hapa nchini kuanzia mwezi ujao ili kupata mafanikio makubwa zaidi ya haya.
Colaso pia akitoa shukrani kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara na Taasisi zake zote kwa kuiunga mkono Airtel Tanzania kwa kipindi chote cha uongozi wake. “nashukuru kwa dhati serikali kwa kutuunga mkono Airtel Tanzania, ndio maana tumefanikiwa kutoa huduma bora kimataifa na hapa nchni sana sana kwenye huduma za Airtel Money, Airtel yatosha bando inayowafaidisha wateja kwa huduma za kupiga simu pamoja na intaneti. Nawapongeza pia wafanyakazi wote wa Airtel kwa kuwa na mafanikio ya kipekee ya kuweza kusambaza huduma za Airtel Money mpaka vijijini ambapo hadi sasa mmefungua zaidi ya maduka ya Airtel Money Branches 900. Alisema Colaso
Mkurungenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alimpongeza Colaso huku akisema mbali ya bosi huyo kuwa ni mtu mwenye maono ya kuendeleza sekta ya mawasiliano hapa nchini, lakini pia alijipambanua katika kuifanya sekta ya mawasiliano kuleta tija katika maswala ya uchumi hapa nchini.
“Tunamuaga leo Mkurugenzi Sunil Colaso, alikuwa ni mtu wa kupenda kazi yake, kujitolea kusaidiana na wafanyakazi kila alipohitajika, alipenda kufanya kazi kwa Umoja, haya ni kati ya mambo ambayo tutamkumbuka nayo. Alikuwa ni mtu mwenye sifa zote za kiongozi na mwenye kujenga timu ya pamoja, alimpa kila mfanyakazi wa Airtel Tanzania nafasi ya kuonyesha uwezo wake.’ Singano alieleza.
Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akipokea keki kama ishara ya kuagana na wafanyakazi wenzake wa Airtel katika hafla maalum kumuaga ilifanyika jijini Dar es salaam baada ya kuiongoza Airtel Tanzania kwa muda wa zaidi ya miaka 6.
Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akikata keki kama ishara ya kuagana na wafanyakazi wenzake wa Airtel katika hafla maalum kumuaga ilifanyika jijini Dar es salaam baada ya kuiongoza Airtel Tanzania kwa muda wa zaidi ya miaka 6.
Bw. Sunil Colaso ametoa wito kwa wafanya kazi na wadau wengine kumuunga mkono Mkurugenzi mpya George Mathen anayetarajiwa hapa nchini kuanzia mwezi ujao ili kupata mafanikio makubwa zaidi ya haya.